Dominika ya 22 ya Mwaka C, 31 Aug 2025

Masomo

Somo la I Yosua bin Sira 3:17- 20, 28 – 29
Katikati Zab. 68: 3 -6, 9-10

Somo la II Ebrania. 12: 18 -19, 22-24

Injili Luka 14: 1, 7-14

MATANGAZO

  1. Tunawashukuru sana jumuiya ya Anna waliosafisha kanisa jana. Idadi yao ni 17 Wiki ijayo ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Karol Lwenga wakifuatiwa na Jumuiya ya Mt. Fransisko Xaveri.
  1. Zoezi la Tegemeza Kanisa linaendelea kwa kasi ndogo. Tunazihimiza Jumuiya zote kuhakikisha uwepo wa ushiriki wa Wanajumuiya kukamilisha kutoa ahadi na kuendelea kupunguza ahadi hizo. Hitimisho la utekekezaji wa ahadi ni mwishoni mwa mwezi Oktoba. Muda uliobaki ni mfupi sana, hivyo viongozi wa Kanda na Jumuiya tunawaomba kufuatilia zoezi hili kwa karibu kuanzia sasa.
  1. Baba Askofu Simon Masondelo, Mlezi wa Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania, anawaalika wana kwaya na waamini walei, kwenye Kongamano la kwanza la UKWAKATA, litakalofanyika Jimbo Kuu la Dodoma, kuanzia tarehe 11 hadi 14 September 2025. Gharama za ushiriki ni shilingi 90,000 kwa wanaohitaji malazi na shilingi 50,000 kwa wasiohitaji malazi. Kwa maelezo zaidi tafadhali uwasiliane na Uongozi wa UKWAKATA Parokia.
  1. Katekista Yohane Maboko mbaye amehudumu katika Parokia yetu kwa muda mrefu, ametimiza miaka 25 ya Ukatekista. Hivyo siku ya Ijumaa tarehe 05/09/2025 saa 11:00 Jioni tutamshukuru Mungu pamoja naye kwa Misa Takatifu ya Jubilei ya miaka 25 hapa Kanisani.
  1. Baba Paroko ametutaka wote wana Parokia kama tunao wazee sana au wagonjwa sana ambao wana upungufu wa Kisakramenti na katika uzee au ugonjwa wao tunaona kuwa hali zao sio njema sana basi tumshirikishe mapema ili aweze kuwasaidia wapate Sakramenti wanazostahili kuliko kusubiri hadi wanapotutoka na kuanza kuhangaika kuomba Misa ya mazishi wakati tunajua kuwa walikuwa na changamoto. Hivyo tujitahidi kuwasaidia wenzetu mapema.Wenye Wazee/ wagonjwa wenye changamoto hizo wafike kuonana na Baba Paroko Ofisi kwake.
  1. Wajumbe wa Halmashauri ya Walei Parokia wanaombwa kuhudhuria mkutano maalum Dominika ijayo ya tarehe 7/09/2025 mara baada ya Misa ya Pili kwenye chumba cha kawaida cha Dalmanutha. Tafadhali wajumbe wote tunaombwa kuhudhuria na kufika kwa Wakati.
  1. Uongozi wa Parokia umetangaza zabuni za kuonyesha nia ya kutoa ushauri wa kitaalamu (expression of interest) wa Miradi ambayo ilitangazwa kwa wanaparokia. Kampuni zenye utaalam na nia ya kushiriki katika zabuni hizo wafike ofisi ya Parokia muda wa kazi kuanzia jumatatu tarehe 1/09/2025, kuchukua nyaraka za zabuni. Gharama za nyaraka za zabuni ni shilingi 100,000. Mwisho wa kuwasilisha nyaraka hizo ni tarehe 8/09/ 2025 Kwa maelezo ya kina tunaomba kusoma katika ubao wa matangazo.
  1. MATANGAZO YA NDOA

TANGAZO LA I

Geoffrey Mwesiga Lwakatare na Leokadia Edward Ngwenge

Francis Evarist Mwalongo na Digna Kitwanga

Danton Niza Mwakyusa na Anjelina Simon Amandus

TANGAZO LA III

  • Imani Hilton Halinga na Maria Goreth Issa Makene
  • Gregorius Ambeiyerelwa na Esther Tito Gollani
  • Julius Bahati na Evelyne Maria
  • Victor Clmence Mushi na Victoria Justine Mtui
  • Sospeter Nestory Msimbe na Neema Epimarck Ombella
  • Philbert Mbezi na Flaviana Libent
  • Aloyce James Mwanga na Kanisia Meinrad Komba
  • Sixbert Mashine Robert na Rose Owden Nsasu
  • Samson Philbert na Irene Hendry Kimaro

MATOLEO:  

      Domnica ya 21 ya Mwaka      5,445,700/= Usd  114, Kshs.2450, Rand 250, Yuan  100 Rupee 20.  

      UWAKA                                    846,400/=

      WAWATA                                860,800/=

      Matoleo ya kila siku.              3,414,250/=

      Zaka                                        4,795,000/=

     JUMLA KUU                       17,069,200/= Usd  114, Kshs.2450, Rand 250, Yuan  100 Rupee 20

    

 ASANTENI SANA KWA UKARIMU WENU NA MUNGU AWABARIKI.